Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Nabi: Tumejiandaa kutinga robo fainali

Nabi Mali 1024x1024 Kocha Nabi

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi mzunguko wa tano (5) kati ya Yanga sc dhidi ya Us Monastir, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kwamba wamejiandaa vizuri kisaikolojia kuhusiana na mechi ya kesho na kuhakikisha wanapata matokeo.

Akizungumza kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Jumapili, majira ya saa 1:00 jioni katika Dimba la Mkapa, Nabi amesema; "Tunajua Monastir wamekuja kucheza mpira na kutafuta matokeo mazuri, sisi kama Yanga tumejiandaa vizuri, kuanzia utimamu wa mwili, kisaikolojia, kimbinu na utayari wa mchezo.

"Wachezaji na benchi la ufundi tumejiandaa kikamilifu, tupo tayari kwa mchezo wa kesho. Tuna uhakika tutapata matokeo mazuri kesho ambayo yatatupeleka hatua inayofata ya robo fainali,"

Us monastir anashika nafasi ya kwanza katika group D akiwa na jumla ya alama 10 huku Yanga sc akiwa nafasi ya pili na jumla ya alama 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: