Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri awachimba mkwara mzito Vipers "Hamuogopi?"

Moses Phiri Ctl Phiri

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa keshokutwa Jumanne, staa wa kimataifa wa Simba raia wa Zambia, Moses Phiri amechimba mkwara mzito kuwa ni lazima washinde kwa hali yoyote, hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuujaza uwanja.

Simba Jumamosi ya wiki iliyopita wakicheza ugenini nchini Uganda dhidi ya Vipers, waliibuka na ushindi wa bao 0-1 kwenye mchezo wa Kundi C kunako Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Simba hatua ya makundi ya mashindano hayo msimu huu ambao umewafanya kufikisha pointi tatu na kupanda mpaka nafasi ya tatu ya msimamo kutoka mkiani walipokuwa awali.

Kabla ya hapo, Simba walipoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Horoya ugenini (1-0) na Raja Casablanca nyumbani (0-3).

Akizungumza nasi, Phiri alisema: “Tumepata pointi tatu za mchezo wa ugenini, ulikuwa mchezo mgumu kwetu kutokana na mazingira ya kucheza ugenini, lakini jambo kubwa ni kuwa tulifanikiwa kupata ushindi wa kwanza na pointi tatu muhimu.

“Mchezo wa Jumanne ni muhimu kwetu kwani ni kama rasmi tumeanza safari yetu ya kufuzu hatua ya robo fainali, tunahitaji ushindi na tutapambana kushinda mchezo huu na iliyosalia ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu kama timu ya kucheza nusu fainali ya mashindano haya.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: