Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri: Simba inataka ushindi tu, si vinginevyo!

Phiri X Jose L Phiri: Simba inataka ushindi tu, si vinginevyo!

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Moses Phiri amesema malengo yao ni kushinda mchezo wa Jumamosi dhidi ya Power Dynamos ya nyumbani kwao Zambia

Phiri ambaye ameondoka na kikosi cha Simba leo kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo, amewatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa yeye pamoja na wachezaji wenzake wataenda kujituma kwa ajili ya matokeo mazuri

"Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwetu kwa sababu watakuwa nyumbani lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda.

"Uzuri ni kwamba ninakwenda kucheza kwenye mazingira ya nyumbani ambako nimekulia, lugha yao wanayozungumza ninaijua, kwa hiyo kwa namna moja au nyingine kutakuwa na urahisi.

"Niwatoe hofu mashabiki, Simba tunakwenda kupambana na sisi kama wachezaji hatuna jambo jingine zaidi ya kutaka ushindi," amesema Phiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: