Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri, Baleke ngoma nzito Simba

Moses Phiri Goals.jpeg Baleke, Phiri wakaliwa kooni

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imebaki saa chache kabla ya Simba kuingia uwanjani leo kuvaana na Vipers ya Uganda katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameendelea kukomalia mastaa wake mazoezini akitaka kutengeneza nafasi na kuzitumia ili kuwarahisishia kazi Kwa Mkapa.

Katika mazoezi ya timu hiyo ya Msimbazi yaliyofanyika juzi jioni kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, kumeshuhudiwa benchi la ufundi likipambana kuhakikisha wanawatuliza wapinzani wao juu kwa juu kwa washambuliaji wao kuwakaba mabeki wasianzishe mashambulizi.

Robertinho aliugawa uwanja na wachezaji kucheza robo uwanja kisha aligawa mabeki na washambuliaji huku akisisitiza zaidi kwa Moses Phiri, Jean Baleke, John Bocco na Kibu Denis kufunga mabao, huku viungo wakabaji na mabeki wakilazimishwa kutumia akili zaidi.

Kikundi cha kwanza kilichoanza kilikuwa na washambuliaji Saido Ntibazonkiza, Nassor Kapama, Clatous Chama, Mzamiru Yassin na Jean Baleke na kwenye upande wa mabeki walikuwa Shomari Kapombe, Henock Inonga, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Sadio Kanoute.

Kikundi cha pili kilikuwa na Isarel Mwenda, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Mohamed Outtara na Erasto Nyoni huku upande wa washambuliaji ni Bocco, Peter Banda, Jimmyson Mwanuke, Habib Kyombo, Ousmane Sakho na Mohamed Mussa.

Katika zoezi hilo ambalo lilikuwa linachukua dakika 10 kwa kila kikundi, washambuliaji waliofunga ni Chama aliyefunga mara mbili, Jean Baleke mara moja na hawa wote walikuwa kwenye kundi moja.

Mshambuliaji mwingine ambaye alifunga bao kwenye mazoezi hayo ni Mohamed Mussa ambaye alipiga shuti nje ya boksi, chipukizi huyu licha ya bao hilo alionyesha bado ana uchu kwani alikuwa akipiga mashuti nje ya lango mara kwa mara.

Katika mazoezi hayo, Moses Phiri alipata nafasi ya kupiga penalti baada ya Mzamiru Yassin kufanyiwa madhambi na Tshabalala na ndipo Phiri alienda kupiga penalti golini akiwa Aishi Manula lakini alipiga nje.

MABEKI WAMALIZA UTATA

Baada ya mazoezi kumalizika Robertinho aliwapumzisha wachezaji wote pembeni na kupanga koni kisha aliwaita mabeki wa kati, Erasto Nyoni, Mohamed Outtara, Kennedy Juma na Henock Inonga.

Kisha akawaita mabeki wa pembeni Shomari Kapombe na Tshabalala pamoja na kipa Aishi Manula kisha aliwataka hawa wapembeni wapige frii-kiki na krosi kisha mabeki akiwa mmoja mmoja kwa nafasi yake alitaka wacheze mipira.

Robertinho aliwataka mabeki hao wawe wepesi na walikuwa wanazunguka koni kabla ya kucheza mpira kwa kuokoa kwa kichwa au mguu na kocha alionyesha kuvutiwa na namna ambavyo walivyokuwa wanaokoa kwa wakati tofauti.

Katika zoezi la kufunga kwa kutumia krosi, Inonga, Outtara na Onyango walifunga huku Kennedy mpira wake ukiishia mikononi kwa Aishi Manula.

Wakati huo huo mshambuliaji Kibu Denis na kiungo Ismail Sawadogo walikuwa wanafanya mazoezi ya peke yao kwa kukimbia wakizunguka uwanja wakati wenzao wakiendelea na programu nyingine.

Kibu alionekana akiwa amevaa kitu kwenye goti lake lakini Sawadogo yeye alikuwa haonyeshi kuwa na mejaraha yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: