Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pale kwa Bangala panamfaa Kanoute

Kanoute Sadio Ss Pale kwa Bangala panamfaa Kanoute

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga wanalazimika kusajili kiungo mkabaji kwenye dirisha hili endapo kiungo wao mahiri Yanick Bangala ataondoka kwenye timu hiyo.

Siku chache kabla msimu haujamalizika, Kanoute alinukuliwa akisema kuwa mkataba wake na Simba umemalizika na katika mazungumzo yao hawajafikia muafaka.

Huyu ni kati ya viungo mahiri wageni ambao wameonyesha kiwango cha juu kwa kipindi chote alichotumika kwenye kikosi cha Simba, akiwa anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wasomi zaidi hapa nchini.

Kanoute raia wa Mali anaweza kuwa msaada sahihi kwa Yanga kwenye eneo la kiungo kama watazungumza naye akiwa na uzoefu mkubwa kwenye ligi kuu, tofauti na yule atakayekuja na asubiriwe hadi azoee, lakini atapunguza gharama kwao kwa kuwa atapatikana bure sokoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: