Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacha ya Mzamiru na Kanoute haifanyi kazi - Oruma

Kanoute, Ngoma Mzamiru Pacha ya Mzamiru na Kanoute haifanyi kazi - Oruma

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya Soka nchini kutoka kituo cha radio cha EFM, Wilson Oruma 'Mzee wa Jambia' amesema kuwa pacha ya viungo wakabaji wa Simba, Mzamiru Yasin na Sadio Kanoute haifanyi vizuri ikilinganishwa na ile ya Mzamiru na Fabrice Ngoma.

Oruma amesema kuwa Kocha wa Simba, Robertinho ana kazi ya kuhakikisha anateua wachezaji sahihi watakaompa matokeo kwenye mchezo wao wa keshokutwa Oktoba 1, 2023 dhidi ya Power Dynamos kwenye Dimba la Azam Complex.

“Hakuna wasiwasi wa Simba SC kwenda hatua ya Makundi, ni kazi ya Kocha kuchagua wachezaji sahihi na mbinu zinazofaa. Partnership ya Mzamiru na Sadio Kanoute pale katikati ni kama imegoma lakini Mzamiru na Ngoma angalau wanafanya vizuri nah ii ni kutokana na uwezo wa Ngoma kuituliza timu, uwezo mzuri wa kupiga pasi.

“Kuna wakati akianza Kanoute na Mzamiru inamlazimu hata Clatous Chama kuondoka kwenye eneo ambalo anakuwa hatari zaidi, anashuka chini ili kuchukua mipira kuwapelekea washambuliaji. Lakini akianza Ngoma anaweza kupokea mipira kutoka kwa mabeki na kuanzisha mashambulizi kwa kupiga pasi nyoofu kwenda kwa Chama na kwenda kutengeneza nafasi,” amesema Oruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: