Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana jana alivurugwa - Shaffih Dauda

Onana Simba Sd Onana jana alivurugwa - Shaffih Dauda

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amesema kuwa, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba, WIlly Onana jana alikuwa amevurugwa kwenye mchezo wao dhidi ya Singida Fountain Gate.

Dauda amesema hayo baada ya mchezo huo kumalizika huku Onana akishindwa kuisaidia timu yake kupata ushindi katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii haki iliyowalazimu Simba kusubiri mpaka mikwaju ya penati iliyowavusha.

"Onana jana alikutana na mechi ngumu sana! Nafikiri akikaa kuitazama mechi ya jana ataona namna ambavyo Yusuph Kagoma alivyomnyima nafasi ya kuonesha ubora wake.

"Ilifika wakat Onana akawa hachezi tena mpira, alikuwa anapiga vikumbo tu kwa sababu tayari walishamvuruga. Kama kungekuwa na VAR bila shaka angekula ‘umeme’ mapema tu akaenda nje," amesema Dauda.

Onana raia wa Cameroon amesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Rayon Sports ya Rwanda ambapo amekuwa akipewa matumaini makubwa ya kuisaidia timu yake kutokana na kiwango chake kuwa bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: