Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana aitabiria Simba ubingwa msimu huu

Onana Simba Sd Onana aitabiria Simba ubingwa msimu huu

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji Simba SC, Willy Essomba Onana ameshukuru kwa kupewa mapokezi mazuri na imekuwa kama bahati kwake kuanza msimu na kombe la kwanza Ngao ya Jamii.

Onana amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Fainali ya Ngao ya jamii jana katika Dimba la CCM Mkwakwani Tanga ambapo timu yake iliibuka mshindi kwa changamoto ya mikwaju ye penati dhidi ya wapinzani wao, Yanga Sc.

Onana akizungumza na wanahabari alisema kuwa anatarajia kuisaidia timu yake ya Simba ili iweze kurejesha makombe yote ambayo yako mikononi mwa Yanga.

Aidha, Mcameroon huyo pia amekubali ligi ya msimu huu itakua ngumu maana timu zote zimejipanga ila Simba ameitabiria kuwa Bingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: