Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana: Nimewasikia mtaona mziki wangu

Baleke Onana Onana: Nimewasikia mtaona mziki wangu

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba kinajifua kimya kimya katika Uwanja wa MO Simba Arena, japo jana kilitarajiwa kuibukia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku mshambuliaji mpya Mcameroon Willy Onana akisisitiza kuwa amewasikia wote wanaomchambua na sasa wataona mziki akirudi uwanjani.

Onana aliyejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Rayon Sports ya Rwanda, amezua mijadala mitandaoni tangu aanze kucheza Bongo ambapo baadhi ya watu wanaamini aina yake ya uchezaji inaigharimu Simba, huku wengine wakimponda anacheza ‘soka laini.’

Mwanaspoti limemtafuta Onana kuulizia jambo hilo na kufunguka kwamba amewasikia mashabiki na wadau wanaojadili aina yake ya uchezaji na analifanyia kazi.

“Nimesikia na nalifanyia kazi, najua Simba ina mashabiki wengi wanaoipenda sana timu yao. Hivyo wanachokitaka ni kuona wachezaji wao na timu inafanya vizuri,” alisema Onana, mwenye bao moja kwenye ligi na kuongeza;

“Nipo hapa kutimiza malengo ya klabu, nitajitahidi kufanya kila liwezekanavyo ili tufikie kile tulichokipanga na mashabiki watafurahi naamini,” alisema.

Onana na Mcameroon mwenzake, Che Fondoh Malone wamekuwa wakifanya mazoezi ya ziada mara kadhaa kwa pamoja lakini pia wamekuwa sambamba na timu kwenye mazoezi ya jumla.

Simba itarejea uwanjani tena kwenye mechi za kimashindano, kati ya Septemba 15-17, itakapocheza mechi ya mkondo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia, ikianzia ugenini.

Kutokana na kuwepo kwa muda mrefu bila mechi, kocha wa kikosi hicho, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameuomba uongozi umtafutie mechi tatu hadi nne za kirafiki huku akisisitiza kati ya hizo, mbili ziwe za timu za Ligi Kuu, huku kukiwa na taarifa huenda ikaenda kujichimbia nje ya jijini la Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: