Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nini utakikumbuka kwa hawa miamba?

Kaze 886 Nini utakikumbuka kwa hawa miamba?

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii miamba kwenye picha ‘Ili kidhi mahitaji’ ya Wananchi kwa maana ya malengo waliyojiwekea na hilo halina ubishi kwani mara kadhaa baadhi ya viongozi wamekuwa wakikiri hilo.

Hitaji la Wananchi lilikuwa ni kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu, Azam Sports Federation Cup (FA) pamoja na Ngao ya Jamii nakufanya vizuri kwenye Michuano ya Afrika na hivyo viliwezekana chini ya hii miamba.

Yanga chini ya Kocha Nasreddine Nabi, Msaidizi wake Cedric Kaze, Mtaalam wa viungo Helmy Gueldich waliweza kuwapa furaha kweli kweli mashabiki wa timu hiyo na huwenda likawa Benchi la Ufundi Bora zaidi kuwahi kutokea Young Africans kwa maana ya kuiwezesha Klabu hiyo Kongwe kufika hatua ya Fainali ya Michuano Mikubwa kabisa Afrika, Kombe la Shirikisho.

Rais wa Yanga Eng. Hersi Saidi akifunguka mafanikio waliyopata kwenye wakati wake wa Uongozi ambao kwenye Benchi la Ufundi lilikuwa chini ya Nabi.

Eng. Hersi Said ”Jukumu letu la kwanza uwanjani ilikuwa ni kuhakikisha tunaleta mataji, changamoto yetu ya kwanza ilikuwa Ngao ya Jamii iliyochezwa mwaka 2022, wote mnakumbuka Fiston Mayele alitetema kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Simba SC na kufanikiwa kubeba.”

Hersi ”Baada ya hapo ilikuwa ni kuupigania Ubingwa wa Ligi Kuu na baada ya hapo Young Africans iliibuka na Ubingwa wa NBC kwa mwaka 2022/23 na kuweka historia ya kufikisha Unbeaten 49 ambazo ni kwa mara ya kwanza katika nchi yetu ya Tanzania.”

”Tukaendelea na jukumu linalofuata, nalo lilikuwa ni mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2022/23 na leo niwathibitishie kuwa Young Africans iliibuka kidedea kwa kuwafunga Azam FC goli 1-0 lililofungwa na Kennedy Musonda katika Jiji la Tanga na kutawazwa kuwa mabingwa.”

”Tukasema msimu huu ni wetu kwenye michuano ya Kimataifa, tukasema mwaka huu lazima Afrika itutambue, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Medali ya kwanza ya CAF Cofederation Cup imetua katika ardhi ya Tanzania kupitia klabu moja tu Young Africans Sports Club.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: