Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nini kilichomkiuta Denis Nkane pale Yanga?

Nkane Denis Dd Dennis Nkane

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Biashara United ilikuwa sehemu ambayo kila kijana aliamini anaweza kwenda kuonyesha uwezo wake na akapewa nafasi kisha safari yake ikaanzia hapo,, tulimuona Novatus Dismas akitengeneza utawala kwenye eneo la kiungo, kilichobaki ni historia tu.

Baada ya kuondoka kwa Nova, Biashara United ilimtambulisha kijana mdogo wao wakamfananisha na kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga Mrisho Khalfan Ngassa, huyu ni Denis David Nkane, moja ya vijana wadogo wenye vipaji vikubwa hapa nchini.

Kiwango chake kiliwashawishi mabosi wa Yanga, akajiunga nao, japo hajapata wakati mzuri ndani ya kikosi hicho kutokana na majeraha ya mara kwa mara lakini anaendelea kuwa miongoni mwa wachezaji hatari wanapopata nafasi ya kucheza.

Nkane alibadili namba ya jezi kutoka 16 msimu uliopita hadi 40 msimu huu lakini bado kiwango chake hakijarejea kama alivyokuwa pale Biashara United, inawezekana msimu huu akafanya vizuri zaidi mbele ya kocha Miguel Gamond.

Changamoto ya Nkane ni nini? Namba ya Jezi aliyoanza nayo ilikuwa kubwa sana kwake au hofu ya kucheza timu kubwa ?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: