Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimemkuta Fei Toto kwenye hali mbaya kiakili - Jasmine

Fei Toto A0012 Nimemkuta Fei Toto kwenye hali mbaya kiakili - Jasmine

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimamizi wa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto', Jasmine Razack amesema amamkuta mchezaji huyo akiwa katika hali mbaya kiakili kufuatia sakata lake la kutaka kuvunja mkataba na klabu yake hiyo kisha kugonga mwamba.

"Mimi nimekuta Feisal ameshatuma barua Yanga sikuwanae tangu mwanzo, lakini nilimkuta katika hali mbaya ya kiakili ni Mchezaji mwenzake wa Taifa Stars alimwambia aje kwangu.

"Kulikuwa na moto hapo kati unawashwa na watu, nilichoamua nikamwambia twende UMRAH kwa sababu niliamini tukifika Makkah kuna ibada kidogo ataweza kutua mzigo. Tulivyorudi akaenda timu ya taifa ingawa hakuwa na mazoezi sana lakini angalau.

"Mkataba wa mchezaji unavunjika wakati wowote, AWE na SABABU au ASIWE na SABABU, hii ni haki ya mchezaji, weka mkataba pembeni ni haki yake .."

"Ukiwa na mkataba utasema umevunja kwa sababu ipi hata kama huna sababu, makubaliano ya pande mbili yataangaliwa lakini kumrudisha mchezaji akatumikie mkataba wake hairuhusiwi"

"Nilichogundua Wachezaji wengi wanaogopa kuwa na wasimamizi kwa sababu wanawalipa pesa, nikawauliza mnawalipa agents wenu kwa nini? Agents wanatakiwa walipwe na klabu sio nyie"

"Kanuni ya 74.14 kwenye kanuni za (TFF) inasema kwamba 'Endapo kuna mgogoro kati ya klabu na Mchezaji chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba ni kamati ya sheria na hadhi za Wachezaji', Nilishangaa sana kwa sababu ni kitu ambacho kinakinzana na sheria za FIFA, haiwezekani Third party avunje mkataba"

"Feisal hajaongea na chombo chochote cha habari hadi sasa , kwahiyo kulikuwa na moto hapo kati unawashwa na Watu, nilichoamua nikamwambia twende Umrah kwa sababu niliamini tukifika Makka kuna ibada kidogo ataweza kutua mzigo,"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: