Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimeikataa Al Hilal nikaja Yanga - Konkoni

Konkoni 177185 Nimeikataa Al Hilal nikaja Yanga - Konkoni

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhsmabuliaji mpya wa Klabu ya Yanga, Hafizi Konkoni amesema kuwa kabla ya kutua kwa miamba hao wa soka, alikuwa amefikia hatua za mwisho za kumalizana na Al Hilal ya Sudan.

Konkoni amesema hayo wakati akihojiwa na Yanga TV, Kambini Avic Town na kuongeza kuwa yeye atafanya kazi yake kama Konkini na si kama Mayele kwa sababu Mayele amefanya makubwa ndani ya klabu hiyo na yeye atafanya kwa uwezo wake kufikia malengo ya Klabu.

Konkini (23) amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea Bechem United FC ya Ghana ambayo ameitumikia kwa miaka saba.

"Nilipoletewa ofa na Yanga nikasema waoooh! Ni jambo zuri kwa sababu ni klabu niliyokuwa ninaifuatilia sana. Nilikuwa nimekaribia kusajiliwa Al Hilal, lakini nikasema acha niende Yanga kwa sababu ni klabu nzuri na itakuwa platform nzuri kwangu.

"Siwezi kutabiri nitafunga mabao mangapi msimu ujao lakini kadri nitakapopata nafasi ya kufunga nitafunga ili kuipeleka timu yangu mbele zaidi na kufikia malengo ya klabu yangu kabla ya malengo yangu. Mashabiki wawe wavumilivu nitafanya vizuri na nitawafurahisha Wananchi," amesema Konkoni.

Mashabiki wengi wa Yanga wanatamani mchezaji huyo awe na uwezo kama Fiston Mayele ambaye ameondoka na kuacha alama kubwa klabuni hapo ambapo kwa misimu miwili amefunga mabao 54 na kuisadia timu yake kubeba mataji 6 ya ikiwemo Ligi Kuu mara mbili na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: