Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni kweli Kapombe aligoma kufanya kazi na Israel Mwenda?

KUMALIZA BIFU Ni kweli Kapombe aligoma kufanya kazi na Israel Mwenda?

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi kutoka Klabu ya Simba zinasema ilikuwa ni kazi ngumu sana kwa mlinzi wa kulia Shomari Kapombe kuongeza Mkataba Mpya klabuni hapo bila uongozi wa Simba kufuata anachotaka yeye, kwa kuwa tayari alishakuwa Ofa ya klabu ya Azam mkononi ila kwanza aliwapa kipaumbele Simba SC.

Maagizo ya Kapombe ndani ya Simba ni kwamba Uongozi Uchague jambo moja, asalie Israel kikosini ama asalie yeye (Shomari),

Israel abadilishiwa namba: Uongozi wa klabu ya Simba ulikaa chini na Israel Mwenda na kumuomba kuwa kuanzia sasa atakuwa anatumika kama Mbadala wa Mohamed Hussein (3) na Sio Shomari kapombe kwakuwa Simba Sc walishawakosa Walinzi wa kushoto waliokuwa wanawahitaji wao (Kibabage ambaye ametua Yanga na Mbegu ametua Singida),

Endapo Israel angegomea hilo basi ilikuwa Lazima aachwe klabuni ili Shomari kapombe aongeze mkataba Mpya,

Kwa sasa usishabgae kuona kwenye Wachezaji wa akiba Duchu na Mwenda wote wakiwepo jua wapo katika nafasi tofauti za kiuchezaji Uwanjani.

Je tukio hili lina faida kwa Timu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: