Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni Kijani, nyeusi na njano kwa Mkapa

IMG 4173.jpeg Ni Kijani, nyeusi na njano kwa Mkapa

Sun, 28 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wananchi wameitika ndicho unachoweza kusema ikiwa zimesalia saa chache kabla ya Yanga kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Ni rangi za kijani, nyeusi na njano ambazo zinaonekana kutawala kwa Mkapa, Wananchi wanaonekana kuwa tayari kushuhudia timu yao ikiandika historia.

Ni maeneo machache mno ambayo yanaonekana kuwa wazi na kwa dalili zinavyoonekana kulingana na idadi ya mashabiki ambao wapo nje ni wazi kuwa uwanjani utajaa dakika chache zijazo.

Hakika huu ni mchezo wa fainali, Wananchi wapo na furaha huku vikundi mbalimbali vya ushangiliaji vikionekana kuanza kazi mapema.

Tayari kocha wa viungo wa Yanga na wa makipa wapo kwenye eneo la kuchezea ili kuweka sawa mambo kabla ya nyota wa timu hiyo kuingia uwanjani kujiweka Sawa na mazoezi madogomadogo kabla ya mchezo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: