Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nasreddine Nabi na hadithi ya Samaki mkubwa kumla Samaki mdogo

Nabi Mds Nasreddine Nabi na hadithi ya Samaki mdogo kumla Samaki mkubwa

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nassirdeen Nabi ameondoka Yanga SC. Haishtui sana. Hatujui kesho na keshokutwa ataondoka staa gani mwingine wa Yanga SC.

Kila Yanga SC ilivyokuwa inafanya vyema nje na ndani ndivyo ilivyokuwa inatengeneza ushawishi kwa timu za wakubwa kutamani mastaa wao. Ndicho kinachotokea sasa. Mastaa wao ni hot cake mezani kwa wakubwa.

Timu kubwa ziko kwa ajili ya kuzidhohofisha timu ndogo, Siku zote iko hivi. Ni kama katika bwawa la samaki kulivyo.

Samaki mdogo huliwa na samaki mkubwa. Yanga SC wameathiriwa na kuwa samaki katika bwawa kubwa dhidi ya samaki wakubwa.

Kocha wao Nabi angeweza kuongeza mkataba mwingine, lakini kuna mahala kapata ofa yenye ushawishi mkubwa na mzuri.

Hapa ndiko kunakoweka tofauti ya timu zetu dhidi ya wakubwa. Unadhani Al Alhy ya Misri hawamtamani staa wa Mamelodi Sundown Peter Shalulile?

Wanamtamani sana, lakini unawaingiaje Mamelodi kirahisi rahisi kumtaka staa wao? Ni kazi ngumu ambayo Al Ahly lazima wajipange nayo. Sio kazi ndogo.

Lakini Shalulile angekuwa mchezaji wa Simba SC na Yanga SC nadhani muda mrefu angekuwa ameshatimka zake nchini.

Nguvu ya fedha inawapa unyonge wakubwa wetu kuwazuia wachezaji na makocha wao muhimu pindi wanapotakiwa na timu kubwa.

Timu zetu zina ushawishi mdogo mezani. Ni tofauti na timu kubwa ambazo kulipa ada nzuri za usajili na kutoa mishahara minono kwao sio shida.

Huu ni unyonge unaouma. Simba SC walikuwa na timu imara Afrika miaka kadhaa iliyopita. Wakubwa walipoanza kugawana mastaa wao, Mnyama hata ubingwa wa ndani anautafuta kwa tochi hivi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: