Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namba ya jezi ni mali ya klabu - Ahmed Ally

Mkude Che Fondoh A0215 Namba ya jezi ni mali ya klabu - Ahmed Ally.

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa jezi ni mali ya Klabu hivyo suala la kustaafisha jezi ya aliyekuwa mchezaji wao, Jonas Mkude lipo chini ya klabu na si mchezaji husika.

Ahmed amesema hayo baada ya jezi aliyokuwa akivaa Mkude ambaye ametimkia Yanga SC, kupewa beki Mcameroon, Che Fondog Malone ikiwa ni siku chache baada ya Simba kutangaza kuwa jezi hiyo wataistaafisha.

"Mkude tutamuaga Simba SC, wewe njoo kwenye Tamasha la Simba Day utaona Mkude akiagwaLakini pia sisi hatuna shida na Mkude. Jezi namba 20 aliyokuwa anaivaa tumempa kijana mwenzake kutoka timu B, Ahmed Ferouz Teru ambaye nae kampa kaka yake Che Malone Fondoh. Namba ya jezi ni mali ya klabu," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: