Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namba 6 ameshawasili Yanga - Kamwe

Screenshot 20230707 195121 Opera News Namba 6 ameshawasili Yanga - Kamwe

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema yule mchezaji namba sita anayezungumziwa kwa wiki kadhaa, tayari amewasili nchini

Kamwe amesema mchezaji huyo pamoja na wengine watatambulishwa baada ya taratibu za ndani kukamilika

"Mchezaji namba sita tayari amewasili nchini, tunapozungumza wakati huu mchezaji huyo yupo katika mikono salama ya Yanga. Hivyo mashabiki wakae tayari kumpokea mchezaji mkubwa"

"Tumeandaa utaratibu wa utambulisho wake pamoja na wenzake. Tulimtambulisha Nickson Kibabage kwa heshima ya mwaliko tuliopewa na Serikali ya Malawi, lakini upo utaratibu tuliandaa na tutautumia katika kutambulisha wachezaji wetu"

"Tunasubiri kocha wetu mkuu (Miguel Gamondi) awasili, tunatarajia atatua nchini Ijumaa (leo) na baada ya hapo tutatangaza benchi la ufundi"

"Kisha tutaanza kuwatambulisha wachezaji wapya akiwemo namba sita ambaye utambulisho wake tumeufanya kuwa wa mwisho," alisema Kamwe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: