Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha Kaizer: Yanga ni timu kubwa, tutawapa heshima wanayostahili

Itumeleng Khune Nahodha wa kaizer, Itumeleng Khune.

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa kaizer, Itumeleng Khune amesema kuwa wanatambua ukubwa na ubora wa Klabu ya Yanga ikiwemo kucheza fainali ya CAF msimu uliopita, hivyo watawapa heshima wanayostahili.

Khune amesema hayo mara baada ya kikosi chao kuwasili nchini usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki katika Sherehe za Kilele cha Wiki ya Mwananchi utakaopigwa kesho katika Dimba la Mkapa, Dar es Slaam.

"Asanteni sana kwa makaribisho yenu, si mara ya kwanza kuja Tanzania, tuliwahi kuja hapa kushindana kwenye michuano ya CAFCL na Simba Sc ambayo ni timu kubwa, Yanga pia ni timu kubwa ambayo imefika mpaka fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Tunawapa heshima wanayostahili Yanga.

"Sisi pia tunajiandaa na msimu mrefu unaokuja, kwa hiyo tutapambana kuhakikisha tunaonyesha tulichokiandaa. Kaizer ni klabu kubwa Afrika Kusini na ina mashabiki wengi, kwa hiyo hatutawaangusha mashabiki wanaoutusapoti kwa sababu tukishinda mechi hii itatupa mwanga mzuri wa kuanza msimu mpya 2023/24.

"Tunajua itakuwa ni mechi kubwa kutokana na ukubwa wa timu zote mbili, Yanga wana ubora mkubwa kwenye kushambulia na wamechukua mataji yote Tanzania msimu uliopita, kwa hiyo itakuwa ni kipimo sahihi kwetu," amesema Khune.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: