Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi kavurugwa, atoa kauli nzito Yanga

Nabi Robertinho Er Nabi kavurugwa, atoa kauli nzito Yanga

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga leo imeondoka nchini kwenda Nigeria ila jana Nabi Mohamed alijifungia na wachezaji hao na kusemana.

Katika kikao hicho kilichofanyika kambini Nabi aliwasema wachezaji hao kwa kumwambia kila mmoja udhaifu wake na makosa yake kwa ukali, lakini akawapa na nafasi wao kujieleza.

Kabla ya kikao hicho mastaa kadhaa wa Yanga, akiwemo Bakari Mwamnyeto, Kennedy Musonda na Fiston Mayele waliomba radhi kwa mashabiki na viongozi kwa njia mbalimbali.

Nabi amelisema kupoteza dhidi ya Simba bao 2-0 wikiendi iliyopita ni yeye na benchi lake la ufundi pekee wanaojua nani alikuwa bora uwanjani na nani hakuwa bora na tatizo lilikuwa nini.

"Mimi na wasaidizi wangu na wao wachezaji tunafahamu nani alifanya makosa, kuna mambo tulielekezana kabla ya mchezo lakini bado makosa yakatokea na sasa yameigharimu klabu lakini huu ni mchezo wa soka kuna wakati makosa yanaharibu hesabu," alisema huku akisisitiza wataivaa Rivers United ugenini wakiwa na mzuka tofauti kabisa.

Nabi ameridhishwa na hatua ya baadhi ya wachezaji wake ambao wamejitokeza hadharani na kuwaomba radhi mashabiki wao akisema hatua hiyo itawarudisha haraka katika njia ya ushindi kwenye mechi zao zijazo.

"Kitu kinachoniumiza ni kila nikikumbuka ule umati wa mashabiki wetu waliokuja kwa wingi wakiamini hatutawaangusha lakini ikatokea kinyume, hii inanipa deni kubwa na nimefurahi kuona hata wachezaji nao wameona wapi wamekosea na kuamua kuwaomba radhi mashabiki wetu," alisema Nabi ambaye mastaa wake wamepoteza Sh400 mil kwa kupoteza mchezo huo.

"Bado tuna nafasi ya kubadilisha mambo, bado kuna mechi zaidi zinakuja ambazo tunatakiwa kuonyesha makosa ya namna hii hayajirudii tena, kuna mechi huko mbele tutazitumia kuwaomba radhi mashabiki wetu kwa vitendo," aliongeza Nabi ambaye Mwanaspoti linajua kikosi chake kinaondoka Dar es Salaam Alhamisi kwenda Nigeria kuwakabili Rivers kwenye Shirikisho.

Wakati huo huo nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job, amesema sasa wamejiweka kwenye wakati mgumu kwa kuwa ubingwa upo wazi.

Yanga inaongoza ligi kwa pointi 68 ikiwaacha watani wao Simba kwa pointi tano ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kukusanya 63, wote wamebakiza mechi nne ili kumaliza msimu.

"Poleni mashabiki tunaumia wote tumekosea hatuwezi kurudia makosa kwenye michezo iliyobaki tutapigana hadi tone la mwisho kuhakikisha tunatetea taji na kufanya vizuri kimataifa matokeo tuyasahau japo tunafahamu kuna utani tunaubeba kama changamoto tunasonga mbele.

"Ulikuwa mchezo mgumu na bora makosa tuliyoyafanya waliyatumia vizuri na kufanikiwa kupata matokeo tunafahamu tumekosea tunajipanga upya na kurudi kwa nguvu lengo letu bado ni kutetea taji pamoja na kwamba sasa tumeongeza ugumu kwa kuwa wigo wa pointi umepungua," alisema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: