Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi azitaka pointi za Simba

AZIZ NA NABII Kocha Nabi

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo wao ujao dhidi ya Simba kwa lengo kuweza kusogelea ubingwa kwa pointi nyingi.

Nabi ametoa kauli hiyo ikiwa Yanga inaongoza ligi kwa pointi 65 ikiwa na tofauti ya pointi tano na wapinzani wao Simba wanakamata nafasi ya pili kabla ya mchezo wa jana wa Yanga dhidi ya Kagera Sugar.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa kila mchezaji wa timu hiyo anapaswa kutambua umuhimu wa kupata matokeo katika mchezo wao dhidi ya Simba kwa lengo la kuongeza pengo la pointi nyingi zitakazoweza kuamua ubingwa kwa haraka.

“Muda uliopo ni mdogo kulingana na ratiba ilivyokuwa ngumu na yenye mechi nyingi lakini tunahitaji kuona tunapata matokeo katika kila mchezo ili tuweze kufikia malengo ya ubingwa kwa kupata pointi nyingi kutokana na kushinda mechi zetu.

“Unajua siyo jambo rahisi lakini kila mchezaji anatambua umuhimu na ukubwa wa kuweza kushinda mechi ambazo zimebakia na ikizingatia tuna mechi ngumu ya watani wa jadi dhidi ya Simba, hatuwezi kuwa na presha lakini kinachotakiwa ni kuona tunaongeza nafasi ya kupata pointi nyingi kabisa,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: