Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi azidi kuitingisha Yanga

Nabi Machozi Kiume Nabi azidi kuitingisha Yanga

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kama ambavyo ilikuwa inazungumzwa kwamba Nasreddine Nabi alikuwa mguu sawa kuachana na Yanga ili kwenda Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na sasa imekuwa rasmi baada ya kocha huyo kukubaliana na mabosi wake, lakini hali hiyo imewatikisha Wanajangwani.

Taarifa ya Yanga kuachana na Nabi ilitolewa juzi usiku na kufanya baadhi wachezaji, wanachama na mashabiki sambamba na wadau wa klabu hiyo kuguswa, kutokana na imani na matumaini makubwa waliyokuwa nayo kwa kocha huyo ilivyowashtua na wengine kutoa maoni yao na kumuaga rasmi.

Nabi alitua Yanga Aprili 21 na kuanza kuiongoza timu kwenye Ligi Kuu bara dhidi ya Azam FC Aprili 25 na kupoteza mechi kwa bao 1-0 lililofungwa na Prince Dube dakika ya 86 baada ya hapo ilibaki kuwa historia, ikiwamo kubeba mataji sita tofauti yakiwemo mawili ya Ligi Kuu, mawili ya ASFC na Ngao ya Jamii mara mbili, mbali na kuifikisha Yanga katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mashabiki wameonyeshwa kuguswa sana na hili lakini kwa wachezaji ambao walikuwa wakiishia na Nabi muda mwingi kwa kipindi chote alichohudumu wao ndio wameonekana kuumia zaidi.

Wachezaji wengi wa Yanga wamemuaga Nabi kwa hisia, wengine wakielezea ukarimu wake na jinsi alivyoishi nao kama baba na siyo kocha tu.

Ukiondoa hao wachezaji, wadau wa soka wakiwemo wachezaji wa zamani na makocha wa timu shindani za ligi Tanzania Bara wametoa yao ya moyoni kutokana na kuondoka kwa fundi huyu wa mpira aliyeacha alama zitakazochukua muda kufutika Jangwani kwani beki Dickson Job aliandika;

"Ulikuwa kama Mwalimu, Baba na rafiki siku zote nilijua kucheza lakini ulinifundisha namna ya kushinda, daima utabaki kuwa Kocha wangu na sitoweza kushukuru kiasi cha kutosha kwa mema yote ulionifanyia kwaheri ya kuonana Baba Nabi." Straika Kennedy Musonda, aliandika;

"Nilikuwa najua kucheza ila umenifundisha jinsi ya kushinda asante sana, umekuwa Baba, Kaka na rafiki mzuri kwangu nakutakia safari njema kwenye Klabu yako mpya asante kwa kumbukumbu nzuri."

Clement Mzize aliandika; "Asante kwa kuniamini na kunipenda sina cha kusema ila ndani ya moyo wangu unaishi, Nakutakia mafanikio mema na asante sana Baba." Farid Musa aliandika kwa ufupia mno; "Kila la heri Baba Nabi", ilihali Fiston Mayele naye aliandika; "Kila la heri Professa kwenye Klabu yako mpya."

Kwa upande wa Sure Boy aliandika; "Ulikuwa wakati mzuri kufanya kazi na wewe Kocha,kila la heri katika majukumu yako mapya Professa,", wakati kiungo Khalid Aucho aliandika;

"Umekuwa Baba, Kaka na rafiki mzuri kwangu nakutakia safari njema kwenye Klabu yako mpya asante kwa kumbukumbu nzuri." Kibwaba Shomari ambaye amekuwa akitumika chini ya Nabi kama beki wa kulia na kushoto kwa vipindi tofauti alisema;

"Ulikuwa sio mwalimu tu bali mzazi na rafiki wa kunifanya niwe imara na kunipa matumaini nma kunifundisha kwernye kila hatua niliyopiga kutimiza ndoto zangu, ikawe heri kwenye changamoto yako mpya Baba Nabi."

Hadi anaondoka, inaonyesha tangu alipofungwa na Azam kwenye mechi ya kwanza, Nabi aliiongoza timu hiyo kwenye mechi 67 na kushinda 52 kutoka sare 13 na kupoteza mbili dhidi ya Ihefu na Simba, huku kimataifa ameingoza kwenye mechi 20 zikiwamo sita za Ligi ya Mabingwa na 14 za Kombe la Shirikisho akiifikisha fainali iliyopoteza mbele ya USM Alger kwa sheria ya bao la ugenini.

DAMIAN MASYENENE, MWANZA MAFANIKIO ya Yanga msimu huu kwenye mashindano ya kimataifa yamemuibua kocha wa zamani wa Biashara United na Tunduru Korosho, Amani Josiah ambaye amesema soka la Tanzania lipo kwenye uelekeo sahihi huku akizipa mtihani wa kubakisha wachezaji wao muhimu na makocha ili kuendeleza walipoishia.

Josiah ambaye ni sehemu ya waanzilishi wa Biashara United, aliliambia Mwanaspoti mafanikio ya Yanga kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza, na kiwango bora ilichoonyesha Simba kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca vinapaswa kulindwa ili kuwa na mwendelezo.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa ufundi Pamba SC ya Mwanza, alisema Simba na Yanga zinaweza kutikisa soka la Afrika kama watawabakisha makocha na wachezaji wao bora na kuongeza wachezaji wa kuwavusha kila hatua waliyokwama.

“Simba na Yanga wanaweza kutikisa soka la Afrika kama wakiyatunza mazuri waliyonayo klabuni wakibakisha makocha wao walionao, wachezaji wao bora kikosini kisha wakaongeza wachezaji wa kuwavusha hapa walipoishia,” alisema Josiah na kuongeza;

“Nadhani soka la Tanzania lipo kwenye uelekeo sahihi kabisa tena linakuja kwa kasi ya juu zaidi tunaweza kuona utawala wa soka la Afrika ukitoka hapa nyumbani, Simba ina nafasi nzuri ya kuchalenji nusu fainali hadi fainali kwa misimu inayokuja endapo wakitizama wapi walipofikia na waimarishe wapi.”

“Nimewatizama Yanga msimu mzima na kwenye fainali niliwaona nadhani wameongezeka ubora kinyume hata na matarajio ya wao wenyewe, kiufundi utaona kuna wachezaji wa daraja la juu zaidi wanahitajika kikosini na siyo wengi nadhani ni eneo la kiungo na mawinga wenye ubora zaidi ya waliopo.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: