Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awapongeza Simba

Nabi Mali 1024x1024 Nabi awapongeza Simba

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameipongeza Simba SC kwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la Klabu Bingwa Afrika (CAFCL) baada ya kuichapa Horoya goli 7-0 na kufikisha alama 9.

Nabi ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu yake ya Yanga na US Monastir ambapo Yanga wameibuka na ushindi wa goli 2-0 na kufikisha alama 10 zinazowafanya wafuzu moja kwa moja kwenda hatua ya robo fainali pamoja na Us Monastir.

"Nawapongeza wanachama na mashabiki wa Yanga kwa kuendelea kuiunga mkono timu katika nyakati zote hadi leo hii tumefuzu hatua ya robo fainali pia naipongeza Simba kwa kufuzu kwenda robo fainali ni vizuri kwa sababu inaonyesha mpira wa Tanzania unakua," amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: