Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awapa Mayele, Musonda siri mpya za Inonga Simba

Srg Mayele Musonda Mayele na Musonda

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kueleka kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewaweka chini washambuliaji wake, Kennedy Musonda na Fiston Mayele na kuwaambia kuwa wanatakiwa kutambua ubora wa safu ya ulinzi ya Simba inayoongozwa na Henock Inonga.

Nabi amefanya kikao na mastaa hao kuelekea kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kupigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar kutokana kutambua ubora wa mabeki wa Simba wanapokutana na timu hiyo.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa ameamua kuwaweka kikao wachezaji hao kwa kuwa anatambua presha ya mchezo huo pamoja na mabeki wa wapinzani wao ambao wamekuwa wakicheza kwa kujiamini wanapokuwa wanakutana nao.

“Tunaendelea na mazoezi (juzi) tulikuwa na program ya gym na leo (jana) tutaendelea na program nyingine kulingana na mchezo ambao tunaenda kucheza kwa sababu tunajua utakuwa na presha kubwa hasa kutokana na matokeo ya mwisho kutoka kila upande.

“Lakini nimejaribu kukaa na washambuliaji wangu na kuwaambia hii ni mechi ya kawaida kama zilivyokuwa mechi nyengine lakini wanatakiwa kutambua ubora wa safu ya ulinzi wa Simba kwa sababu hawapaswi kujenga taswira ya kilichotokea kwenye mechi zao zilizopita, zaidi watanakiwa kuongeza nguvu na juhudi za kutakiwa kujua wanawezaje kuifungua na kupata ushindi,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: