Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awaomba radhi Yanga "Hatukufungwa sababu ya mvua"

Nabi X Aziz Ki Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi.

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewaomba radhi mashabiki na wananchama wa timu hiyo baada ya kupata matokeo mabaya kwenye mchezo wao wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirkisho Afrika dhidi ya USM Alger uliopigwa wikiendi iliyopoita katika Dimba la Mkapa na Yanga kupokea kichapo cha bao 2-1.

Nabi ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar kabla ya kuanza kwa safari ya kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Nabi ameongeza kuwa anao uhakika kutokana ubora wa kikosi chake, hivyo watapata matokeo chanya na kurejea na ubingwa huo nyumbani.

“Kwanza niwaombe radhi mashabiki na wananchama wa Yanga kwa matokeo ya juzi, hata sisi tumeumia sana lakini ndiyo matokeo ya soka.

“Hatukufungwa kwa sababu ya mvua, kwani timu zote zimecheza na mvua, tulifungwa kutokana na presha ya mchezo kuwa kubwa zaidi. Kwa sasa tumesahahu na akili yetu kwa sasa ni kuhusu mchezo wa marudiano kule Algeria.

“Nimeshazungumza na wachezaji wote, wana ari kubwa ya kuutaka ushindi wa mchezo huo, uwezo wao ninaujua, iwapo watajitoa kwa asilimia 100 ninaamini tutapata matokeo. Wachezaji wameniambia wapo tayari kujitoa kwa asilimia 200, ni jambo jema na tunaamini tutaweza.

“Kiufundi, tunazo mbinu ambazo tumejiandaa kwenda kuwakabili, tunajua mchezo utakuwa ni mgumu ikizingatiwa itakuwa ugenini, kwa hiyo tumejiandaa vizuri kwa hilo, ila siwezi kuanika silaha zangu kwa adui,” amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: