Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awajaza upepo Mayele, Musonda

Musonda Mayele Ghs Nabi awajaza upepo Mayele, Musonda

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amesema hataki kuona wachezaji wake wakibweteka, kwani bado wana kibarua kigumu.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0, yakifungwa na washambuliaji wake, Kennedy Musonda na Fiston Mayele.

Ushindi huo umewafanya Yanga wakae kileleni katika msimamo wa Kundi D wakiwa na pointi 10 sawa na US Monastir wakifuatiwa na Real Bamako (5) na TP Mazembe (2). Yanga na US Monastir zimefuzu robo fainali.

Akizungumza nasi, Nabi alisema wachezaji wake hawatakiwi kubweteka kwa sasa na badala yake wanatakiwa kujituma katika kuipambania timu yao ili iendelee kufanya vema katika michezo ijayo ukiwemo wa mwisho wa hatua ya makundi watakaocheza ugenini dhidi ya TP Mazembe.

Nabi alisema kufuzu kwao hakuwafanyi waudharau mchezo huo dhidi ya TP Mazembe, kwani ndio utakaowafanya wamalize michuano hiyo wakiwa kileleni katika Kundi D. “Sitaki kumuona mchezaji wangu yeyote akibweteka baada ya kufuzu robo fainali kwani bado tuna kibarua kigumu mbele ya wapinzani wetu TP Mazembe.

“Mchezo huo tunatakiwa tumalize kwa ushindi ili tuendelee kukaa kileleni katika msimamo wa kundi letu ambalo tunapata ushindani kutoka kwa US Monastir.

“Hivyo ili tukae kileleni ni lazima tuwafunge TP Mazembe nyumbani kwao, nafahamu itakuwa ngumu, lakini nitaendelea kukiboresha kikosi changu katika baadhi ya maeneo ili makosa yaliyotokea mchezo uliopita hayajitokezi tena,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: