Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi awabadilishia gia TP Mazembe

YANGA NABI Vg Kocha Nabi

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, anatarajiwa kuwabadilishia mbinu wapinzani wake, TP Mazembe kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa kila mchezo una mbinu zake jambo ambalo linamfanya abadilishe kila wakati kuwakabili wapinzani.

“Tumefanikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali na bado tuna mchezo mmoja ambao ni muhimu, ili kupata matokeo mazuri ni lazima tubadili mbinu za ushindi.

“Aina ya wachezaji pamoja na kazi ambayo tutaifanya hasa kwenye kuboresha makosa ambayo tumefanya kwenye mechi zilizopita ni muhimu kufanya kazi kubwa.

“Kujituma na nidhamu ni jambo la msingi kwa kila mmoja, tunaamini tutafanya vizuri kwani wachezaji wapo tayari na tunahitaji kufanya vizuri,” alisema Nabi.

TP Mazembe inatarajiwa kuwakaribisha Yanga, kesho Aprili 2 kwenye mchezo utakaochezwa nchini DR Congo wakati Yanga ikiwa tayari imefuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na US Monastir.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: