Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi ataja watakaoikosa TP Mazembe

Nabi Mali 1024x1024 Nabi ataja watakaoikosa TP Mazembe

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kuifuata TP Mazembe kesho, Alhamisi kikiwa na majembe yake kamili, Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Nasreddine Nabi.

Ametaja wachezaji wawili ambao hawatakuwa sehemu ya mpango wa mchezo huo wa kukamilisha hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga tayari imefuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na inachokitafuta kwa sasa ni kushinda na kumaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi lao la D, wakati huu ikikalia nafasi hiyo kutokana na kuizidi US Monastir ya Tunisia kwa tofauti ya mabao tu ya kufunga na kufungwa baada ya timu hizo kila moja kuwa na pointi 10.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe, hivyo mchezo ujao utakaochezwa DR Congo Jumapili wiki hii kila timu itakuwa na kazi ya kusaka pointi, lakini hata kama miamba hiyo ya Congo itashinda bado Yanga na US Monastir itakayocheza na Real Bamako, ndizo timu zilizofuzu hatua ya robo fainali.

Akizungumza nasi jana, Nabi aliwataja wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya msafara wa timu hiyo kuelekea DR Congo, kuwa ni Bernard Morrison na Denis Nkane.

Alisema licha ya wachezaji hao kuanza mazoezi baada ya kupona majeraha yao yaliyowaweka nje kwa muda mrefu, hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachondoka Alhamisi kuelekea DR Congo katika dhidi ya wenyeji wao, TP Mazembe.

Aidha, alisema umakini na ushirikiano wa wachezaji wake utakuwa mkubwa utakaowapa nguvu kuongoza kundi lao, kwa kuwa bado hawajamaliza kazi.

Alisisitiza kuwa wachezaji wake wanapaswa kuendelea kujituma na kuongeza juhudi zaidi kuelekea katika michezo ya robo fainali kwani watakutana na timu kigogo zaidi kutoka hatua ya makundi.

“Tumefika hatua ya robo baada ya miaka mingi, ni hatua ngumu tunayokwenda kucheza, wachezaji wanatakiwa kuongeza umakini na kujituma zaidi kwa kuanza kutumia mechi dhidi ya TP Mazembe, kama sehemu ya kujiandaa na michezo ya robo na kusaka pointi tatu,” alisema kocha huyo raia wa Tunisia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: