Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi ashtukia jambo Marumo, Musonda, Mayele wapewa kazi maalum

Yanga 04 Nabi ashtukia jambo Marumo Gallants

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameshtuka mapema baada ya kuwaambia washambuliaji wake, Fiston Mayele na Kennedy Musonda kuwa, wanapaswa kuhakikisha wanaimaliza mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ndani ya dakika 45 kwa kufunga mabao ya kutosha ambayo yawavusha kirahisi.

Nabi amelazimika kutoa kauli hiyo kwa washambuliaji hao kufuatia Simba kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco kutokana na kushindwa kupata ushindi mkubwa nyumbani.

Mei 10, mwaka huu, Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, kisha marudiano ni Mei 17, 2023 nchini Afrika Kusini.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuna kila sababu ya washambuliaji wake kuhakikisha wanapamba kumaliza mechi yao ya nusu fainali ndani ya dakika 45 kwa lengo la kupunguza presha kuelekea mchezo wa marudiano.

“Siku zote watu wanajifunza kutokana na makosa yao au watu wengine ambayo husaidia kuwa bora kutokana na mikakati bora wanayoweka jambo ambalo tumeliangalia kwa namna kubwa katika mchezo wetu wa hapa kwa sababu matokeo ya mapema yanasaidia kukuweka salama zaidi ikiwa wachezaji wanajua wajibu wao.

“Hatuhitaji kuona tunacheza kwa presha yoyote kwenye mchezo wetu wa hapa zaidi ya kuona safu ya ushambuliaji inatumia nafasi zote muhimu kufunga mabao mengi katika dakika 45, hiyo ndiyo itakuwa salama ya kupunguza presha katika mchezo ujao kwa sababu ikiwa tutashindwa kufanya hivyo hapa basi tutakuwa tumerudia makosa ya wapinzani wetu,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: