Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi amtega Robertinho Yanga

Nabi X Kaze Ahadi Nabi amtega Robertinho Yanga

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefunguka kuwa anatambua kwa sasa mahesabu yao ni kuhakikisha wanapata pointi sita ili kutangaza ubingwa lakini itawabidi wahakikishe wanapata ushindi katika mechi mbili zijazo ikiwemo ya Simba inayonolewa na Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ili kufikia malengo yao.

Nabi ametoa kauli hiyo licha ya Yanga kukabiliwa na michezo miwili muhimu ya Kombe la Shirikisho ambapo keshokutwa Jumapili wanatarajia kucheza dhidi ya Monastir kabla kuwafuata TP Mazembe katika mchezo utakaopigwa Aprili 2, mwaka huu nchini DR Congo kabla ya kurejea nchini kuwavaa Simba katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Aprili 16, mwaka huu.

Katika msimamo wa ligi, Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 65 ikifuatiwa na Simba wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 huku Singida Big Stars ikishika nafasi ya tatu na pointi zao 48.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa anatambua ukubwa na gumu wa michezo yao miwili ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini haiwafanyi waache kupoteza malengo yao kwenye Ligi Kuu Bara kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Simba kwa kuwa ni sehemu ya ubingwa wao msimu huu.

“Najua kwa sasa tunaangalia mechi hizi mbili katika michuano ya kimataifa kwa sababu tunataka kuona tunaweza kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuhakikisha matokeo makubwa yanapatikana kwenye mchezo wetu na Monastir ambao ndiyo utakuwa ni fainali kwetu ya kuweza kufikia malengo.

“Lakini haiwezi kuondoka kile ambacho kipo mbele yetu hasa upande wa ligi kwa sababu bado hatujashinda ubingwa na mchezo ujao utakuwa dhidi ya Simba ambao wao watakuwa wakitaka kuona wanaweza kutufunga vipi, sisi tunaendelea kubadilika katika kila mchezo utakao kuwa mbele yetu kwa kuhakikisha matokeo yanapatikana,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: