Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi afunguka kuwabadilishia mbinu wapinzani

Kocha Nabi Marumo Gd.jpeg Nasreddine Mohammed Nabi

Mon, 22 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohammed Nabi amesema kuwa alilazimika kuwapumzisha baadhi ya nyota wake katika mchezo wa nusu fainali ya Kombel la Shirikisho la Azam jana dhidi ya Singida Big Stars kutokana na uchovu walioupata kwenye mchezo dhidi ya Marumo Gallants.

Nabi amesema hayo mara baada ya kuifunga Singida Big Stars kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Fiston Mayele akitokea benchi kipindi cha pili na kuifanya timu hiyo itinge fainali ya michuano hiyo.

“Mechi ilikuwa ngumu kwa sababu Singida BS walikuja na mfumo mzuri wa kuzuia na kipindi cha kwanza hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga na hizo chache hatukuzitumia vizuri, hii ni kutokana na uchovu wa wachezaji.

“Tumecehza mechi ngumu ya nusu fainali ya CAF, tumerudi, ilitakiwa kufanyiwa mapumziko kwa baadhi ya wachezaji. Kipindi cha pili nilifanya mabadiliko ambayo yametusaidia kupata matokeo.

“Nilisema kwamba kama tutafunga kipindi cha kwanza, basi wachezaji wenye uchovu tutawapumzisha lakini baada ya kuona ni bila bila mpaka dakika za mwisho ndipo nikapata sub tukapata bao,” amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: