Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi afichua siri nzito Yanga

Yanga Hdkd Nabi afichua siri nzito Yanga

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nasredine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, ameweka wazi kuwa, siri ya kupata ushindi kwenye mechi tisa mfululizo za Ligi Kuu Bara ni kuzungumza na wachezaji kuhusu kutumia nafasi pamoja na nidhamu.

Timu hiyo inaongoza ligi ikiwa na pointi 59 baada ya kucheza mechi 22, ina kibarua cha kutetea ubingwa wa ligi iliyoutwaa msimu uliopita huku ikiwa na rekodi ya timu ya kwanza kushinda mechi tisa mfululizo msimu huu za ligi hiyo.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa kazi kubwa kwenye kusaka ushindi inabebwa na wachezaji ambao wanatimiza majukumu kwa umakini.

“Sio kazi rahisi kuwa hapa lakini ninawapongeza wachezaji licha ya wakati mwingine kutokuwa kwenye kiwango bora bado wanacheza kwa nidhamu na kufuata malekezo.

“Malengo ni kufanya vizuri na ambacho ninawaambia wachezaji ni kujituma na tunaandaa mechi vizuri ili kupata matokeo.

“Ni lazima tuandae mechi kulingana na aina ya mchezo ambao tunacheza na kikubwa ni kuona tunashinda na kupata matokeo mazuri ambayo ni muhimu kwetu.

“Kila timu inahitaji ushindi nasi tunafanya maandalizi mazuri, kila mmoja anaonyesha uwezo wake na kufanya kazi kubwa kwenye kutafuta ushindi,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: