Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi aanika mastaa wa Yanga watakaokosekana leo dhidi ya Monastir

Nasreddine Nabi El Proffessor Nabi aanika mastaa wa Yanga watakaokosekana leo dhidi ya Monastir

Sun, 19 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa leo katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir.

Nabi amewataka mashabiki waujaze uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuwapa nguvu wachezaji wao kuhakikisha wanapambana kuibuka na ushindi katika mchezo ambao wanatarajia kuwa mgumu.

"Nawaomba mashabiki wa Yanga waje kwa wingi uwanjani. Tunataka muwe sambamba nasi, mtushangilie katika nyakati zote. Wachezaji wetu watapambana sana pale mtakapokuwa mnawashangilia kuliko mkiwa kimya.

"Monastir ni timu nzuri hawakuja hapa kutembea najua wamekuja kutafuta matokeo mazuri ili wajihakikishie kuwa vinara wa kundi. Nawapongeza kwa kufikisha miaka 100 siku ya jana, najua kesho watakuja kupambana ili wafanye maadhimisho yao vyema.

"Sisi tumejiandaa kwa ajili ya mchezo huo na lengo letu ni kutafuta ushindi ili tuweze kufuzu robo fainali," alisema Nabi.

Akizungumzia hali ya kikosi, Nabi amesema wachezaji David Bryson, Benard Morrison na Denis Nkane watakosekana katika mchezo huo.

Bryson ni majeruhi wakati Morrison na Nkane wameanza mazoezi mapesi lakini hawako tayari kwa mchezo huo.

Nabi alibainisha kuwa wachezaji Fiston Mayele na Kennedy Musonda walikuwa na majeraha madogo lakini wako tayari kwa mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: