Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi aandaa mbinu za kivita kuwaua Bamako

Nabi Yanga Msd Nabi aandaa mbinu za kivita kuwaua Bamako

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alichokipanga Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ni kuwavurga Real Bamako na kuondoka na alama tatu kwenye mchezo wao wa marudiano kesho Jumatano kwa kutumia mbinu ya kivita.

Nabi amepanga kuwashambulia Bamako kwa haraka na kutafuta angalau mabao mawili kwenye dakika 15 hadi 20 za mwanzo ili kuwachanganya zaidi wapinzani hao kama walivyofanya dhidi ya TP Mazembe.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe alipozungumza na Championi Jumatatu na kuweka wazi mipango ya Yanga kuelekea kwenye mchezo huo wa marudiano baada ya sare ya 1-1 na Real Bamako wiki iliyopita.

“Nabi amesema, anachohitaji ni timu yake kupata mabao ya haraka haraka kwenye mchezo dhidi ya Bamako. Yaani kwenye dakika 15 hadi 20 ubao uwe unasoma 2-0.

“Hivyo ndivyo itakavyokuwa, kwa sababu ukiachana na kocha, hata wachezaji wenyewe wanautaka huo mchezo kuliko kocha mwenyewe. Kwa hiyo itakuwa ni balaa mashabiki waje,” alisema.

Keshokutwa Jumatano Yanga watacheza mechi ya marudiano na Real Bamako, ukiwa ni mchezo wa pili baina yao utakaochezwa kwa Mkapa ukiwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: