Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi aagiza winga Mali

Ousmane Kamissoko 1 Ousmane Kamissoko.

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi akiendelea kuandaa ripoti ya nyota atakaochana nao na kuwaongeza kikosini hapo kwa msimu ujao, ameufahamisha uongozi wa klabu hiyo kuanza kumfuatilia Mshambuliaji wa Real Bamako, Ousmane Kamissoko.

Kamissoko mwenye miaka 24, aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Real Bamako, Julai 1, 2022, ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo amekuwa na kiwango bora msimu huu ambapo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe, Machi 19 mwaka huu alifunga mabao mawili.

Chanzo chetu kutoka Yanga, kimesema kuwa, tayari Nabi ameshaonesha kuvutiwa na ubora wa Kamissoko, hivyo amewataka viongozi wa Yanga, kuanza mazungumzo mara moja na nyota huyo, kama watafanikiwa basi ataachana na Tuisila Kisinda.

“Tunamshukuru sana kocha wetu kwa kuendelea kuwa na jicho la kipekee la kufanya maboresho katika kikosi chetu, pamoja na kuwa bado tuna mechi sita za kukamilisha msimu huu wa ligi, ameuomba uongozi kumfuatilia straika wa Bamako, Kamissoko ili kama watafanikiwa kumshawishi aweze kuja akiwa ni mbadala wa Kisinda,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: