Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Yanga tunajivunia kuwa na Mayele

NABI MAYELE NA AZIZ Nabi: Yanga tunajivunia kuwa na Mayele

Sat, 27 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa fainali ya kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Alger, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema wapo tayari kuwakabili wapinzani wao baada ya kukamilisha aina tatu ya maandalizi kwa ajili ya mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, kocha huyo amesema kuwa maandalizi hayo yaliegemea zaidi kwenye utimamu wa wachezaji, mbinu watakazotumia na kuwasoma wapinzani wao na kujua namna ya kuwadhibiti.

“Ni mchezo mkubwa na mgumu kutokana na maandalizi ya pande zote mbili, kwetu dhamira yetu ni kupata ushindi katika ardhi ya nyumbani, sababu nina mchanganyiko wa wachezajiwengi wazuri wanaotengeneza kikosi bora, akiwemo Fiston Mayele ambaye kwa sasa ni mshambuliaji bora Afrika na tunajivunia kuwa naye Yanga,” amesema Nabi.

Yanga itashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho saa 10:00 alasiri kucheza na USM Alger na inahitaji kupata ushindi, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kubeba taji hilo katika mchezo wa marudiano wiki ijayo nchini Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: