Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Tutawakabili Mazembe kwa nidhamu kubwa

NABI CAF CC Kocha Nabi

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nasreddine Nabi, Kocha wa Yanga, amesema kuwa wataingia kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe kwa nid¬hamu kubwa ili kupata matokeo mazuri.

Yanga ina pointi 10 kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kucheza mechi tano, inaongoza Kundi D ikiwa imetinga hatua ya robo fainali.

Mchezo wa mwisho dhidi ya TP Mazembe, utachezwa kesho Aprili 2, 2023 ambapo Yanga itakuwa ugenini DR Congo. Mchezo wa nyumbani, Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-1.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa ni muhimu kwa mchezo ujao kucheza kwa umakini mkubwa ili kupata matokeo.

“Tumefurahi kwa kufanikisha malengo ya timu kufuzu hatua ya robo fainali, bado kuna malengo yanapaswa kuendelea kutimia ikiwa ni pamoja na ushindi mchezo wetu ujao.

“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni jitihada kwenye maandalizi na kuwakabili wapinzani kwa nidhamu kubwa jambo litakalotupa matokeo mazuri ugenini,” amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: