Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Tumeumia kumkosa Aucho fainali

AUCHOOO Nabi: Tumeumia kumkosa Aucho fainali

Sun, 28 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema Yanga imeumia kumkosa Khalid Aucho katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Nabi amesema hayo Dar es Salaam Dar katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo kwenye uwanja wa Bemjamin Mkapa, Mei 28.

Aucho anatumikia adhabu kutokana na kupata kadi sita za njano.

“Tumeumia kumkosa Aucho lakini hakuna namna, ni suala la kikanuni. Tumezungumza nae na atakuwa na timu kwenye mechi zote mbili kwa ajili ya kuwahamasisha kupata matokeo mazuri,” amesema Nabi.

Hata hivyo amesema Yanga ina bahati kuwa na Fiston Mayele ambaye ni mshambuliaji wa daraja la juu Afrika na kwamba uzoefu wake pamoja na wachezaji wengine utakuwa msaada mkubwa kwenye hatua hiyo ya Fainali.

Naye Nohodha Msadizi wa Yanga, Dickson Job amesema tayari walimu wamewapa wachezaji maelekezo ya nini cha kufanya ndani ya uwanja hivyo kazi imebaki kwao kwenda kupambana ili kushinda mchezo huo.

“”Watanzania waondoe uoga, nawaomba wajitokeze kwa wingi siku ya kesho na kushangilia kwa dakika zote. Vijana wao tuko tayari kwa ajili ya kupambana kuwapa furaha,” amesema Job.

Mchezo wa marudiano kati ya timu hizo utafanyika Algeria June 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: