Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Siko tayari kufungwa mpaka fainali

Kocha Nabi Marumo Gd.jpeg Kocha Nabi akizungumza

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezi wa kesho dhidi ya Marumo Gallants, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema hataki kupoteza mchezo wowote ili afike fainali kwa kishindo pasipo kufungwa.

Nabi amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano na wanahabari nchini Afrika Kusini huku akikiri pia kuwa ingawa mchezo huo utakuwa ngumu lakini amejiandaa na kikosi chake kuhakikisha anashinda.

"Ni jambo zuri Marumo wamepanga mechi isiwe na kiingilio. Sisi kama Yanga tunapenda kucheza mbele ya mashabiki wengi kuliko uwanja kukosa mashabiki. Nina wachezaji wenye uzoefu wa kutosha wa kucheza mechi za namna hii.

"Tumesahau kuhusu faida ya ushindi wa 2-0 tulioupata kwenye uwanja wa nyumbani. Huu ni mchezo mwingine na tuko na mpango mwingine wa dakika 90 za hapa.

“Sitaki kupoteza mchezo Nataka kufika fainali kwa kishindo japo natambua kuwa mechi itakuwa ngumu,” amesema Kocha Nabi.

Yanga watakuwa na kibarua kigumu kesho mbele ya vijana hao wa Madiba kusaka nafasi ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika huku Yanga akiwa na faida ya bao 2-0 alizowafunga Marumo katika Dimba la Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: