Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Msimshambulie, Mzize amecheza vizuri

Mzize Rt.jpeg Nabi: Msimshambulie, Mzize amecheza vizuri

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amemtetea kinda wake, Wari Clement Mzize akisema kuwa alicheza vizuri kwenye mchezo wao dhidi ya Rivers United licha ya kukosa nafasi mbili za wazi jana Aprili 30, 2023 katika DImba la Mkapa.

Nabi amesema hayo mara baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuiondoa Rivers United ya Nigeria huku baadhi ya wadau na mashabiki wa soka wakidai kuwa Mzize hakucheza vizuri kwani ameinyima timu yake ushindi kwa kukosa nafasi za wazi.

“Mimi kwa upande wangu sijaona kama amecheza vibaya, ni kijana wa Kitanzania ambaye tunamtengeneza, ikipatikana nafasi unampa ili uone atafanyaje.

“Alitengenezewa vizuri akapata nafasi mbili, moja ikapita juu na nyingine pembeni, alikuwa kwenye movement na amesaidia pia kukaba. Mimi naona amecheza vizuri kutokana na umri wake jinsi ulivyo,” amesema Nabi.

Wachezaji saba wa Tanzania walioanza kwenye kikosi cha Yanga hapo jana dhidi ya Rivers United;

1. Dickson Job

2. Kibwana Shomari

3. Ibrahim Baka

4. Bakari Mwamnyeto

5. Mudathiri Yahya

6. Salum Aboubakar

7. Clement Mzize.

Yanga itakutana na Marumo Gallants katika hatua ya nusu fainali ambapo mchezo wa kwanza utapigwa katika dimba la Mkapa, Mei 10, 2023 kisha mchezo wa marudiano utapigwa nchini Afrika Kusini Mei 17, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: