Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi, Mayele sio hadhi ya Yanga - Oruma

NABI MAYELE NA AZIZ Nabi na Mayele.

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa masuala ya Soka nchini, Wilson Oruma amedai kuwa aliyekuwa Kocha wa Klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi na mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele hawana hadhi tena ya kuendelea kuwepo klabuni hapo.

Akijibu chapisho la Meneja wa Idara ya Maudhui Yanga, Privaldinho, Oruma amesema Mayele na Nabi thamani yao ni kubwa hivyo si rahisi kuendelea kusalia Yanga.

"Chama na Miquissone waliondoka kwasababu Simba Sports hawakuwa na hadhi tena kuwabakiza. The same imetokea kwa Nabi na itatokea kwa Fiston Mayele.Wamekuwa wakubwa sio HADHI tena ya Yanga Africa.

"Samaki wakubwa wanakula Samaki wadogo always.That is nature uwe UNATAKA au HUTAKI. Sasa ukiandika hivi watu wanakasirika na wanakuja na Makala Juu Kwasababu ni Kawaida yao Kukasirika. Kwenye Football ya Africa sisi team zetu bado tunajitafuta.We are no body.

"Yani haiwezekani Yanga Africa na Simba Sports wawe wanamiliki mchezaji mzuri au Kocha mzuri Halafu Al Ahly, Wydad Casablanca,Raja Casablanca, Mamelodi Sundown nk wakae Kimya tu."

"Watakuja watamtaka na watamchukua tu uwe UNATAKA au HUTAKI. Fiston Mayele hawezi kutakiwa na Kaizer Chiefs, halafu Yanga Africa mkamzuia.Huo uwezo haupo. Ngoja niishie hapo, nikaishi kwanza," amesema Oruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: