Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Doumbia hajaingia kwenye mfumo wangu, apambane

Nabi X Doumbia.jpeg Nabi: Doumbia hajaingia kwenye mfumo wangu, apambane

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga katika dirisha dogo walimsajili Beki Mamadou Doumbia kutoka Mali kwa lengo la kuimarisha kikosi chao.

Tangu kuwasili kwa Mlinzi huyo katika Kikosi cha Yanga, ameshindwa kupata nafasi na kuwafanya wengi kuhoji uwezo wa mchezaji huyo.

Sasa Kocha wa Kikosi cha Yanga, Nasreddine Nabi ametoa kauli kuhusiana na kupata nafasi kwa mchezaji huyo.

Nabi amesema kuwa Doumbia ni mchezaji mgeni hivyo anahitaji kupata muda ili kuzoea mazingira mapya kitu ambacho sio rahisi.

Lakini kubwa kuliko yote Nabi amesema Doumbia bado hajaingia kwenye mfumo wake hivyo anapaswa kupambana sana ili ajihakikishie nafasi katika kikosi cha Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: