Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzize: Ubingwa una maana kubwa kwangu

Clement Mzize Second Goal Clement Mzize

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji chipukizi wa Yanga, Clement Mzize amesema ubingwa waliochukua jana unamaana kubwa katika historia ya maisha yake ya soka la ushindani.

Akizungumza nasi, mshambuliaji huyo amesema mafanikio hayo yatamuongezea ari ya kuzidi kujituma ili aweze kufanya vizuri zaidi siku zijazo akiwa na miamba hiyo ya Tanzania Bara.

“Namshukuru Kocha wangu Nasreddine Nabi kwangu ni kama baba kutokana na ushauri anaonipa lakini pia ni mtu mwenye imani kubwa na mimi hilo linanifanya kuongeza bidii na kujituma ili nimfurahishe,” amesema Mzize.

Mshambuliaji huyo amesema kwa nafasi aliyopewa ataendelea kupambana ili msimu unaokuja aweze kufanya vizuri zaidi ikiwemo kuwa tegemezi kwenye kikosi cha kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: