Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzimu wa Mayele unavyomtesa Konkoni "Nakosa usingizi"

Vn Mayele Hafizi Konkoni afunguka mzimu wa Mayele unavyomtesa

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa Yanga SC Hafiz Konkoni baada ya kufunga goli lake la kwanza tangu ajiunge na Yanga na akilitaja jina la Fiston Mayele, huku akisema imekuwa furaha sana kwake kwa kupewa Hamasa na mashabiki wa Yanga na kifanikiwa kufunga goli moja mbele ya KMC.

Konkoni ambaye ni raia wa Ghana amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza wa Yanga wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC ambapo straika huyo alifanikiwa kufunga bao moja miongoni mwa mabao 5-0 ambayo Yanga ilishinda jana.

“Yanga walikuwa na moja ya washambuliaji bora barani Afrika, Fiston Mayele, mimi kuja kuziba nafasi yake sio kazi ndogo, sote tunajua mengi ambayo amefanya na mashabiki wengi wana matarajio makubwa na mimi.

“Haikuwa kazi rahisi kwa sababu presha ya mchezo ilikuwa kubwa sana kwangu hivyo nilihitaji kufunga bao hili ili kushusha presha hiyo, hii imenipa nguvu na nina hakika nitaendelea kufunga inshallah.

“Mashabiki wananitegemea sana na hasa wakiangalia kile alichokuwa akikifanya Mayele, wanategemea niwafanyie makubwa, kwakweli nakosa usingizi lakini wananipa shauku ya kufanya vizuri zaidi.

Yanga SC wameanza vizuri na mchezo wa kwanza dhidi ya KMC kwa kupata idadi kubwa ya mabao huku mchezo wa pili watakutana na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: