Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Mchachu: Skudu sio mchezaji, ni msanii

Skudu Yanga Ds.jpeg Fiston Mayele

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Simba Sc, Mzee Mchachu amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Skudu Makudubela si mchezaji wa soka badala yake ni msanii wa Bongo Fleva kutokana na tabia yake ya kupenda kucheza muziki.

Mchachu amesema kuwa mchezaji huyo aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini iliyoshuka daraja, hana maajabu ya kisoka badala yake ni mchezaji wa 'shoo off' tu.

"Niliitazama mechi ya Yanga na Kaizer Chiefs, kiukweli mtani alijitahidi ila mimi nimependa zaidi yule kijana wa Ivory Coast (Yao), anaujua.

"Sasa wale wengine huwezi kusema ni wabaya au wazuri ni mpaka watakapozoeana na wenzao na ligi yetu kama unavyojua unatakiwa uwe ngangari.

"Skudu namuona kama mchezaji wa Bongo Fleva tu, amekuja pale anakatika, anacheza, anarusha mpira anaupitisha kwenye mikono, zile ni mbwembwe tu. Kuna mchezaji kama Morrison bwana? Alikuwa anauchezea mpira anaukalia juu.

"Hii ni Ligi ya Tanzania bwana ukiweza kucheza hapa unaweza kucheza hata Ligi Kuu ya Uingereza," amesema Mzee Machachu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: