Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi wa Dabi ya Kariakoo huyu hapa

PostQueueImg 1 62f3c5d8c18d5 Mwamuzi wa Dabi ya Kariakoo huyu hapa

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jiji la Dar es Salaam litasimama kwa muda wikiendi ijayo wakati miamba wawili wa soka la Tanzania watakapovaana kwenye Uwanja wa Mkapa, Simba itakapowakaribisha watani zao Yanga.

Tumezoea kuona majina ya waamuzi yakifichwa lakini safari hii gazeti hili limeweza kuyanyaka mapema majina ya waamuzi wanne watakaochezesha dabi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni alisema tayari majina manne yameorodheshwa kwa ajili ya kusimamia mchezo huo wa Ligi Kuu.

Alisema wameteua waamuzi wanne pekee na sio sita kama ambavyo huko nyuma ilivyokuwa ikifanyika katika dabi ambazo zimekuwa na presha kubwa ya mchezo.

“Tumechagua majina manne ya waamuzi wenye uwezo mkubwa ambao wote wana kitambaa cha Fifa kutokana na kuwepo kwa mwenendo mzuri waliokuwa nao hivi karibuni kwenye ligi.

“Kwa sasa tunangoja kuyaidhinisha na Jumatano yatawekwa wazi ili kila mmoja ajue na tumefanya hivyo kutokana nani viwango vya waamuzi kuongezeka kwa sasa,” alisema Amduni.

Kutokana na kauli ya bosi huyo huku ikifahamika Tanzania ina waamuzi wenye beji ya Fifa kuwa ni 14 na mmoja wapo (Salum Siyah) anachezesha Ligi Kuu ya Zanzibar.

Waamuzi 13 waliosalia wapo Ligi Kuu Bara ambao watano wanachezesha katikati, nao ni Ahmed Arajiga, Ramadhan Kayoko, Tatu Malogo, Jonesia Rukyaa na Hery Sasii.

Kati ya waamuzi hao watano tayari waamuzi wawili walisimamishwa muda mrefu ambao ni Arajiga na Sasii, hivyo waamuzi watatu waliosalia, Tatu Malogo pekee hajawahi kuchezesha dabi.

Kutokana na kauli ya Amduni, bila shaka mwamuzi wa kati anaweza kusimama Kayoko au Rukyaa ndiyo wameonekana kwa siku za hivi karibuni wakitamba.

Kayoko ndiye mwamuzi aliyechezesha dabi iliyopita Oktoba 23 na endapo atasimama kati itakuwa rekodi kwake kwani katika dabi 15 za mwisho hakuna mwamuzi aliyechesha dabi mfululizo.

Mara ya mwisho kwa Rukyaa kuchezesha dabi ilikuwa Januari 4, 2020, wakati timu hizo zikitoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu.

Katika dabi 15, Sasii ndiye mwamuzi aliyehusika mara nyingi (13) akisimama katikati mara mbili na mwamuzi wa akiba akiwa mara 11 wakati, Kayoko akiwa katikati mara nne, akisimama kama mwamuzi wa akiba mara mbili na pembeni mara mbili kwenye michezo ambayo walikuwa waamuzi sita.

Waamuzi wanaochezesha pembeni wenye beji ya Fifa wapo tisa ambao ni Hamdani Ally, Janet Balama Yusuf Hashim, Tesha John, Frank Komba, Soud Lila, Mohamed Mkono, Kassim Mpanga na Rajabu Ramadhan.

Pia Amduni amethibitisha, Arajiga ni miongoni mwa waamuzi watakaopuliza kipyenga cha Afcon U17 mwaka huu baada ya kufanya vyema michuano ya Cecafa U17 mwaka jana na ile michezo ya kufuzu Afcon U17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: