Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto: Fei Toto bado wa moto

Mwamnyeto X Fei Toto Mwamnyeto: Fei Toto bado wa moto

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Yanga kuifunga Azam kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii, nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amezungumzia kiwango cha nyota wa zamani wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ akisema bado wamoto.

“Fei ni mchezaji mzuri na akitua timu yoyote atapewa nafasi ya kucheza bila wasiwasi lakini tunauelewa uwezo wake akiwa uwanjani, hivyo hakuna kilichotusumbua tulipokutana naye Mkwakwani,” alisema nahodha huyo wa Wananchi.

Aidha alisema wachezaji wapya wamekuwa na mchango mkubwa kwa kipindi kifupi walichokuwa nao tangu wasajiliwa na kusema wameongeza kitu kikubwa ndani ya timu hiyo.

“Wachezaji wapya wote ni wazuri ndio maana wamesajiliwa na kila anayepewa nafasi anaitumia vizuri kwa kuonyesha kile alichonacho na wameongeza ushindani mkubwa na mzuri ndani ya timu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: