Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambieni Onana hapa ni Bongo sio Rwanda

Onana Simba Sd Mwambieni Onana hapa ni Bongo sio Rwanda

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwambieni Onana, hapa ni Bongo na hili ni soka la Bongo si la Rwanda, magoli aliyofunga kule Rwanda huku anaweza akafunga mawili tu, ligi yetu ni ngumu sana inahitaji wachezaji wanao weza kufosi na akili mingi, Jasho Jingi

Ila nikimuangalia Onana ni kama ana ka ustaa flan hivi yaani anataka kucheza soka la kistaarabu sana wakati mchezo unahitaji speed.

Yaani kwa namna Onana anavyocheza huyu ni wa kumuingiza dakika ya 85 wakati Team ishashinda goli 4 aingie akatoe tu burudani, mwambieni bwana, ohoooo ustaa ni mwingi kuna muda anapoteza mpira kidhereu sana, halafu harudi kusaidia team inaposhambuliwa.

Mdogo wangu Onana nimekuangalia ila nikwambie tu Soka la Bongo ni la kuvuja jasho, hapo hujakutana na Tanzania Prisons kuna watu wanaitwa kina Asukile , Kwa uchezaji wako wa kistaa kistaa hivyo utamfukuzisha kazi mapema mno mzee baba Tinyo. Umepoa sana kama mchuzi wa mbwa mdogo wangu, changamka hapa ni Bongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: