Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba yuko tayari kununua jezi kwa milioni mbili

Swaleh Suleiman Ahmed Ally.jpeg Mwamba yuko tayari kununua jezi kwa milioni mbili.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa, Swaleh Suleiman yuko tayari kununua Kibegi ama Jezi itakayozinduliwa Ijumaa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa milioni mbili.

“Swaleh Suleiman Madjapa (Mwenye Miwani) yuko tayari kununua Kibegi au Jezi itakayozinduliwa juu Mlima Kilimanjaro kwa Shilingi Milioni 2.”- Ahmed Ally

Mtoto huyo wa Mzee Ally ameongeza kuwa; “Simba tumetangaza kuziuza Jezi zote 6 zitakazozinduliwa Juu ya Mlima Kilimanjaro kwa njia ya mnada.

“Fedha zitakazopatikana kutoka kwenye mnada huo zitapelekwa kwenye ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospital ya Muhimbili.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: