Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba huyu hapa!

Morrison Ds Bernard Morrison

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga mtukutu wa Yanga, Bernard Morrison yuko tayari kurejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi mitatu.

Mara ya mwisho Morrison kuonekana uwanjani akiitumikia Yanga ulikuwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Disemba 23 na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Morrison alishiriki kikamilifu katika kupatikana kwa ushindi huo akitengeneza bao la kusawazisha lililofungwa na Fiston Mayele.

Kiuhalisia Morrison ana deni kubwa kwa uongozi na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa na imani kubwa katika urejeo wake.

Pamoja na usumbufu aliowasababishia Wananchi pale alipotoroka nyumbani, lakini aliporejea walimpokea kwa mikono miwili.Baada ya kupona majeraha, wengi wanatarajia Morrison ataifanya vyema kazi iliyomrejesha Yanga.

Majeraha yalipelekea asiwe na mchango katika mapambano ya kuipeleka Yanga robo fainali ya michuano ya Shirikisho (CAF), anaweza kuwa na mchango kule DR Congo kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao Yanga inahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza kinara wa kundi.

Aidha bado kuna mechi sita za kuhitimisha msimu ambazo anaweza kushiriki pamoja na mechi za kombe la FA Yanga ikiwa hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: